Klabu ya Real Madrid iko mbioni kumalizana na mshambuliaji wake namba moja Karim Benzema ili kumuongezea mkataba mchezaji huyo mpaka 2024.
Real Madrid imepanga kumuongezea nyota huyo mkataba wa mwaka baada ya mkataba wake wa awali kumalizika juni 2023 klabu hiyo inaendelea na utaratibu wa kuongeza mikataba mifupi kwa nyota wake ambao wamefika miaka 30 na kuendelea.
Karim Benzema amekua na wakati mzuri sana ndani ya Real Madrid baada ya kuondoka kwa nyota wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo huku yeye akionekana kuibeba timu hiyo muda mwingi haswa katika msimu wa 2021/22 ambapo alimaliza kama mfungaji bora wa ligi kuu Hispania na Ligi ya mabingwa barani ulaya huku michuano yote klabu hiyo ikatwaa ubingwa.
RealĀ inatarajia mchezaji huyo kubeba tuzo ya Ballon Dor hivo kushehekea tuzo hiyo na mkataba mpaya wa mwaka mmoja.