Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania imepanga kumuongezea mkataba beki wake kitasa Eder Millitao raia wa Brazil baada ya kua na wakati mzuri klabuni hapo.
Beki huyo wa kibrazil aliejiunga na Real Madrid mwaka 2019 akitokea klabu ya Fc Porto ya nchini Ureno ammbapo alicheza kwa msimu mmoja kwa ubora na mabingwa hao wa ulaya kuvutiwa nae na kumsajili mchezaji huyo.
Millitao hakua na msimu mzuri ndani ya Real Madrid katika misimu miwili ya kwanza pamoja na kutokupata nafasi kwasababu ya mabeki waliokuwepo klabuni hapo, kama Raphael Varane pamoja Sergio Ramos ambapo walisababisha ufinyu wa nafasi klabuni lakini baada ya kuondoka wachezaji hao beki huyo alianza kupata nafasi na akawa na msimu bora sana mwaka 2021/22.
Mabingwa hao wa Ulaya wana mpango kumuongozea mkataba mchezaji huyo mkataba mpya mchezaji utakamfunga klabuni hapo mpaka 2028 na wanatarajiwa kuweka kipengele cha €bilioni moja ili kumpata mchezaji huyo.
Millitao amekua miongoni mwa wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha mwalimu Carlo Anchelotti tangu kocha huyo atue klabuni hapo.