Kocha wa klabu ya Atletico Madrid Diego simeone amewataka wachezaji wa timu hiyo kua na utulivu wa akili licha ya kupoteza mchezo wao wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji.

diego simeoneEl Chollo amejaribu kuwatuliza wachezaji wake baada ya kupokea vipigo mfululizo katika ligi ya mabingwa ulaya huku wakishika mkia kwenye kundi B lakini kocha huyo anaamini bado wana wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi.

“Ulikua mchezo ambao tulicheza vizuri, Nafikiri Tulitawala Mchezo na tulihitaji kucheza, Nimeondoka na vitu vingi vizuri licha ya kupoteza” Tuna michezo kadhaa ya kucheza,Tunatakiwa kutuliza akili na hatutakiwi kua na wasiwasi kwasababu kila kitu kiko wazi”

“Tulipata nafasi mara mbili hadi tatu, lakini tulishindwa kupata nafasi ya kufunga huku Brugge wakienda mapumziko wakiongoza” Alisema Diego Simeone

diego simeoneKlabu ya Atletico imekua na wakati mgumu sana kwenye michuano ya Ulaya msimu baada ya kushinda mchezo mmoja mpaka sasa wakiwa na alama tatu huku wakishika mkia kwenye kundi B.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa