Simeone kocha wa Athletico madrid ya nchini Hispania amemwaga misifa kibao kwa mshambuliaji wa klabu wa timu hiyo Antoinev Griezmann.

Hii imekuja baada ya jana nyota huyo raia wa Ufaransa kufunga goli la usiku kabisa kwenye dakika za nyongeza dhidi ya Fc Porto na kuiwezwsha Athletico kupatab ushindi wa goli mbili kwa moja na kuwafanya vijana hao wa Simeone kufungua kampeni za mwaka huu kwa ushindi kwenye michuano ya ulaya.

simeoneKocha huyo hakuweza kuficha hisia zake baada ya mchezo kumalizika na kusema Griezmann ni miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi kwenye historia ya klabu hiyo yenye maskani yake jijini Madrid.

Antoinne Griezmann ni mchezaji ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa mafanikio klabu hiyo ambapo amefanikiwa kucheza fainali za ulaya mwaka 2016 wakifungwa na mahasimu wao Real Madrid pia alikuepo kwenye kikosi cha Athletico kilichobeba ubingwa wa ligi kuu Hispania maarufu kama La liga kwa mantiki hii kocha huyo mtata anakua yupo sahihi kumuelezea nyota huyo wa kifaransa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa