Mkurugenzi na gwiji wa klabu ya Bayern Munchen Oliver Kahn amefunguka na kusema hawafikirii kuhusu kiungo wa klabu ya Borrusia Dortmund raia wa Uingereza Jude Bellingham.

oliver kahnGwiji huyo ameeleza hayo baada ya kua taarifa kua klabu hiyo inafatilia kwa ukaribu kuhusu kiungo huyo anaefanya vizuri kwasasa duniani kutoka klabu ya Dortmund, hii imetokana na klabu ya Bayern kua na ushawishi mkubwa sana kwa wachezaji wanaocheza ligi ya Ujerumani hivo vyombo vya habari kutaka kujua kama ni kweli wanamhitaji mchezaji huyo.

Jude Bellingham anafataliwa na vilabu vingi vikubwa barani ulaya ukiachana na Bayern Munich ambao wamejitoa vilabu kama Real madrid,Liverpool, pamoja na Man United nin miongoni mwa vilabu ambavyo vinawinda saini ya kiungo huyo fundi.

“Hatufikirii kuhusu Jude. Ni kweli ni mchezaji mzuri lakini tuna wachezaji Kimmich,Goretzka,Gravenbach, Sabtzer”. Alisema Oliver Kahn.

oliver kahnWadau wengi hawaamini maneno ya Oliver Kahn kwakua mara nyingi timu hiyo inakanusha kufatilia mchezaji lakini mwisho wa siku wanamsajili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa