Kocha wa klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu nchini Italia Luciano Spalletti ameonesha kufurahishwa na kipigo kizito walichokitoa kwa klabu ya Ajax wakiwa ugenini dhidi ya klabu ya Ajax Amsterdam.

luciano spallettiLuciano Spalletti anaamini hata gwiji wa timu hiyo ya Diego Armando Maradonna angekuepo angefurahi kutoka na ushindi huo mnono walioupata dhidi ya klabu ya Ajax katika uwanja wao nyumbani.

Licha ya Ajax kutangulia kupata bao mapema dakika ya tisa ya mchezo kupitia kwa kinda raia wa Ghana Mohamed Kudus lakini Napoli walirudi na kufunga mabao kupitia Giacomo Raspadori, Di lorenzo, na Piotr Zielinski na kuwafanya Napoli kua mbele kwa mabao matatu kwa moja hadi mapumziko.

Napoli kipindi cha pili walikuja kwa kasi tena na kupata bao la nne kupitia kwa Giacomo Raspadori kabla ya Kvaratskkhelia na Simeone kufunga kila mmoja na kufanya mabao kua sita kwa moja.

Ajax walipata wakati mgumu pia baada ya nahodha wao Dusan Tadic kupata kadi nyekundu katika mchezo huo na kuwafanya Ajax kushindwa kurudi mchezoni kabisa.

Luciano Spalletti amesifia uwezo wa wachezaji wake waliouonesha katika mchezo huo huku wakifata maelekezo yake kwa kucheza mchezo muhimu zaidi.

liciano spallettiNapoli wanaongoza kundi A kwakua wameshinda michezo yote mitatu wakiwa na alama zao 9 katika kundi hilo hivohivo timu hiyo inafanya vizuri katika ligi ya ndani baada ya kua haijapoteza mchezo wowte katika ligi ya nyumbani na kuongoza ligi pia nchini Italia maarufu kama Serie A.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa