Casemiro: "Brazil Ina Nguvu Zaidi Kuliko Mwaka wa 2018"

Casemiro anaamini kuwa Brazil wako katika nafasi nzuri zaidi kwenye Kombe la Dunia la Qatar kuliko ilivyokuwa Urusi mnamo 2018.

 

Casemiro: "Brazil Ina Nguvu Zaidi Kuliko Mwaka wa 2018"

Kiungo huyo wa kati wa Manchester United, Casemiro alitupia  bao la ushindi dakika ya 83 dhidi ya Uswisi hapo jana na kuihakikishia Brazil inakwenda hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia.

Hadi kufikia hatua hiyo kwenye Uwanja wa 974, Brazil ilimkosa mchezaji wake Neymar ambaye aliumia kwenye mchezo wa kwanza huku kikosi hicho kikijuliza kitafanya nini baada ya kumkosa mchezaji huyo.

Brazil ndio timu ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kutofungwa katika mechi 17 mfululizo za hatua ya makundi ikiwa ni pamoja na raundi ya mwisho na ya pili ya makundi katika matoleo ya awali, ingawa ni mara ya kwanza tangu 2010 kwa Selecao kushinda mechi zao mbili za ufunguzi kwenye michuano hiyo.

Casemiro: "Brazil Ina Nguvu Zaidi Kuliko Mwaka wa 2018"

Wakiwa wametinga robo fainali nchini Urusi kabla ya kwenda Ubelgiji, Brazil ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa Qatar, na Casemiro hana shaka kuwa kikosi hicho kina nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa kwenye Kombe la Dunia lililopita.

Amesema kuwa; “Miaka minne imepita, kuna wachezaji wapya, mwaka huu tuna chaguo pana zaidi, tuna zaidi ya kuchagua, bila hata kubadili timu tunaweza kubadilisha uchezaji,”

Casemiro anaamini kuwa hakuna shaka kuwa wana machaguo zaidi kuliko yale ya 2018, na sio tu kwasababu muda umekwenda na wamekomaa, wana mabeki wenye uzoefu zaidi pia wamekuwa na mechi nyingine bila kupoteza.

Casemiro: "Brazil Ina Nguvu Zaidi Kuliko Mwaka wa 2018"

Maoni ya Casemiro yaliungwa mkono na kocha wao Tite, ambaye alidai mshindi wa kweli wa mafanikio ya Brazil Jumatatu ilikuwa “mchakato” wa kuendeleza kikosi cha vijana, huku akisema kuwa kuna chaguzi mbalimbali kwasababu kuna muda wa miaka minne wa kuunda hilo kitu ambacho kimeshinda jana ni miaka hiyo minne.

Brazil wanahitaji pointi moja tu kutoka kwa mchezo wao wa mwisho wa Kundi G dhidi ya Cameroon ili kutinga kileleni, na mechi dhidi ya washindi wa pili wa Kundi H, linalojumuisha Ureno, Ghana, Uruguay na Korea Kusini, katika hatua ya 16 bora.

Haijulikani ikiwa Neymar, ambaye alipata jeraha la kifundo cha mguu katika ushindi wa wiki iliyopita dhidi ya Serbia, atakuwa sawa kucheza dhidi ya Cameroon, lakini Tite alifurahishwa na kwamba Brazil ilifanya kazi hiyo bila kuwa na mchezaji wao bora.

Casemiro: "Brazil Ina Nguvu Zaidi Kuliko Mwaka wa 2018"

Alipoulizwa ikiwa Brazil ilikosa ubora wa Neymar, Tite alisema:  “Ni wazi, Neymar ana ujuzi tofauti, ni mchezaji anayeweza kufanya matukio ya ajabu, na wachezaji wengine bado wanafikia kiwango hicho na ninatumai watafika, lakini acha tufurahie ushindi huu.”


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

kmc

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.