Antonio Conte amesema kuwa wachezaji kumi na wawili wa Tottenham walioshiriki Kombe la Dunia hawatapata muda wa kupumzika kwani Ligi tayari imesharejea.

Spurs watarejea dimbani Siku ya kesho dhidi ya Brentford, siku nane tu baada ya wachezaji wao wawili nahodha wa Ufaransa Hugo Lloris na mlinzi wa Argentina Cristian Romero kucheza fainali ya Kombe la Dunia.
Lloris atakuwa kwenye benchi dhidi ya Brentford lakini kuna uwezekano wa Romero kuwepo kikosini. Spurs pia wanapaswa kukabiliana na kukosekana kwa Richarlison, huku mshambuliaji huyo wa Brazil amepata jeraha baya la misuli ya paja alipokuwa akicheza nchini Qatar.
Son Heung-min, Eric Dier na Harry Kane walitinga hatua ya 16 bora na robo fainali ya shindano hilo wakiwa na Korea Kusini na Uingereza mtawalia, huku Ivan Perisic aliingia ndani kabisa ya shindano hilo na Croatia.

Conte; “Sina furaha kabisa, kwa upande mmoja, una furaha kwa sababu kwa klabu yangu, Tottenham, kuwa na wachezaji 12 kwenye Kombe la Dunia ina maana kwamba tuko katika njia sahihi ya kujaribu kuwa washindani na kujaribu kushinda kitu.”
Haiwezekani kuwapa mapumziko mengi na kwa hakika na wachezaji ambao hawakucheza Kombe la Dunia na wanafanya kazi kwa wiki nne, sasa wako katika hali nzuri ya kimwili.
Conte anasisitiza walifanyia kazi sana kipengele cha mbinu na kipengele cha kimwili. Sasa wako katika kiwango ambacho ni bora zaidi kuliko wachezaji waliomaliza Kombe la Dunia, kwasababu hii anadhani lazima afanye uamuzi bora zaidi kwa mchezo dhidi ya Brentford.

Baada ya kumenyana na Brentford, Spurs watawakaribisha Aston Villa Siku ya Mwaka Mpya kabla ya kumenyana na Crystal Palace Januari 4.

