Klabu ya Simba ipo mbioni kumalizana na na kocha wa klabu ya Horoya ya nchini Guinnea, Kocha huyo ambaye ni raia wa Senegal Lamine N’diaye.
Viongozi wa klabu ya Simba wako katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha dili la kumshusha kocha huyo mwenye uzoefu na soka la Afrika, Inaelezwa kocha huyo anatakiwa kuungana na timu hiyo kuelekea michuano ya Mapinduzi nchini Zanzibar.
Kocha huyo atakuja kuungana na kocha wasasa klabuni hapo Juma Mgunda na yeye atasimama kama kocha mkuu, Huku Mgunda akisimama kama kocha msaidizi kutokana na uzoefu mkubwa aliokua nao Lamine.
Kocha Lamine N’diaye ambaye amewahi kuvifundisha vilabu vya Tp Mazembe, Al Hilal, Pamoja na timu ya taifa ya Senegal na kwasasa akifanikiwa kuifanya Horoya kua moja ya vilabu tishio barani Afrika.
Kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika anakuja ndani ya klabu ya Simba kwajili ya kuliongezea nguvu benchi la ufundi la klabu hiyo kuelekea ligi ya mabingwa Afrika, Ambapo klabu hiyo ipo kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo.

