Klabu ya Simba inaendelea na maandalizi ya Mchezo wa tarehe 26/12/2022 dhidi ya KMC FC unaotarajiwa kupigwa katika Dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Simba imetoka kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera katika mchezo wao uliopita huku wakitarajia kuondoka na pointi 3 CCM Kirumba ili kupunguza gepu lililopo kati yao na vinara wa Ligi Yanga.
Mgunda na vijana wake wanaenda kwenye mchezo dhidi ya KMC wakikumbuka sare ya 2-2 waliyopata kwa Mkapa baada ya vijana jao wa Thiery Hitimana kurejesha mabao ambayo walikuwa wameyafunga.

KMC baada ya kuwa na mwenendo mbaya walirudi relini ambapo walishinda michezo yao miwili mfululizo , huku Msimbazi wataingia dimbani na kumkosa kinara wao wa mabao Mosses Phiri aliyeumia mchezo uliopita.

