Vijana wa Mecky Mexime Kagera Sugar baada ya kutoka kumlazimisha mnyama Simba sare nyumbani kwake, kesho wanatarajia kushuka Dimbani kwao palepale Kaitaba kukiwasha dhidi ya Geita Gold.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 12:15 huku Geita Gold wakitarajia kusaka pointi tatu muhimu ili waweze kujiweka kwenye nafasi nzuri kwani msimu uliopita walimaliza nafasi ya nne.
Kagera Sugar na Geita Gold wanafanana pointi zao kwenye msimamo ambapo wanazo 23, ila kinachowatofautisha ni mabao ya kufunga na kufungwa, huku Mexime na vijana wake wapo nafasi ya 6 na vijana wa Minziro wapo nafasi ya 7.

Mechi ya mwisho kumenyana walitoka sare ya kufungana bao 1-1 huku Walima miwa ndio walianza kufunga na kisha bao hilo likaja kusawazishwa.

