Klabu ya Kagera Sugar ya huko mkoani Kagera leo hii imemtangaza kocha mkuu wa timu hiyo Mecky Mexime ambaye atadumu klabuni hapo hadi mwisho wa msimu2022/2023, baada ya hapo jana kumtimua aliyekuwa kocha wao Francis Baraza.

 

Kagera Sugar Yamrejesha Aliyekuwa Kocha Wao Mecky Mexime

Kagera wamechukua uamuzi huo wa kumrudisha Mexime kutokana na kwamba kocha huyo alishaitumikia klabu hiyo kabla ya mkataba wake kumalizika 2021 na wameona ndiye mtu sahihi wa kuinoa klabu hiyo.

Kabla ya kutangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Mexime alikuwa ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa Stars, lakini pia amevinoa vilabu mbalimbali ikiwepo kile cha Mtibwa Sugar kabla ya kuhamia kwa Wanankurukumbi.

Kagera Sugar Yamrejesha Aliyekuwa Kocha Wao Mecky Mexime

Mexime anaikuta timu ipo katika nafasi ya 13 baada ya kucheza michezo 9 wameshinda mechi mbili, sare mbili na wamepoteza michezo mitano huku wakiwa na pointi 8 tuu ambazo wamejikusanyia.

Wanankurukumbi wana kazi kubwa ya kufanya kwani nafasi ambayo waliyopo ni hatari na wasipoangalia wanaweza kuangukia nafasi ya mwisho. Hivyo kocha huyo ataweza kubadilisha chochote? ambapo mechi ijayo ya Ligi watacheza dhidi ya KMC wakiwa nyumbani kwao.

Kagera Sugar Yamrejesha Aliyekuwa Kocha Wao Mecky Mexime

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa