Klabu ya Namungo hii leo inamkaribisha Kagera Sugar katika mchezo wao wa Ligi kuu ya Tanzania Bara katika uwanja wao wa Majaliwa majira ya saa 1:00 usiku.
Namungo ametoka kupoteza mechi mbili mfululizo kwenye ligi na hivyo zimemfanya awe kwenye nafasi ya 7, baada ya kucheza mechi saba, amecshinda mechi tatu, katoa sare mbili, na ana pointi 11 kwenye Ligi.
Wakati kwa wapinzani wao wa Leo Kagera wao ndani ya michezo 8 waliyocheza, wameshinda miwili, wametoa sare mbili na wamepoteza michezo minne wakiwa wamejikusanyia pointi 8 tuu mpaka sasa.
Mechi ya mwisho kukutana timu hizi, walitoa sare ya kufungana kwa bao 1-1 huku kila mtu akiihitaji mechi ya leo kwa ukubwa zaidi hasa kwa Kagera ambaye bado anajitafuta kutokana na mwenendo wake kwenye Ligi.
Swali linakuja je anaweza kufanya chochote hii leo akiwa ugenini tena dhidi ya Namungo ambao wametoka kujeruhiwa mechi mbili mfululizo? huku wenyeji wao wakiwa tayari kuwavaa na Kagera Sugar.