Privadinho Akanusha Nabi Kuondoka Yanga

MKUU wa Idara ya Maudhui ya Kidigitali wa Klabu ya Yanga SC Priva Abiud Shayo Maarufu kama Privadinho, amewataka mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kupuuza taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kutimuliwa kwa kocha mkuu wa klabu hiyo Nasraddine Nabi.

Privadinho alisema kuwa taarifa yeyote kama haipo kwenye mitandao rasmi ya klabu ya Yanga hiyo inapaswa kupuuzwa.

“Niliwaambia kama haipo kwenye App ya Yanga potezeeni.” Alisema Privadinho kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Kocha Nabi aliwasili Yanga Aprili 21, 2021 na kufanikiwa kuifundisha timu hiyo ambayo, ilichukua ubingwa msimu wa 2021/2022 bila kufungwa, Ubingwa wa Kombe la Shirikisho 2021/2022 na ngao ya jamii mara mbili 2021/2022, 2022/2023.

 

Privadinho Akanusha Nabi Kuondoka Yanga

Sababu iliyokuwa ikielezwa na wengi ambayo huenda ingemuondoa klabuni hapo ni kutofanikiwa kupata matokeo mazuri kimataifa, ikiwemo kushindwa kufuzu hatua ya makundi ya CAFCL, Msimamo wake wa kukataa sajili za baadhi ya wachezaji kama Tuisila Kisinda na Bernard Morrison.

 

Acha ujumbe