NAHODHA wa Mabingwa wa Ligi ya wanawake nchini Tanzania, Simba queens Opa Clement ameushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa wachezaji wote ili kufikia malengo waliyoyaweka ikiwemo kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika upande wa wanawake.

 

Opa Clement Atoa Neno kwa Uongozi Simba SC

Opa aliyasema hayo leo 25 Oktoba, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya safari yao kuelekea nchini Morocco, kwaajili ya kushiriki mashindano ya Ligi ya mabingwa, ambapo timu hiyo inatarajia kuondoka kesho alfajiri kupitia Uturuki na kisha Morocco.

“Tunawashukuru viongozi wetu kwa sapoti kubwa wanayotupatia, wamekuwa wakiweka mazingira yetu ya kazi kuwa rahisi, kikubwa tunawaomba mashabiki waendelee kutuombea ingawa hawatakuwepo uwanjani,” Nahodha Opa Clement

Simba Queens inakuwa ni klabu ya kwanza kutoka Tanzania kushiriki mashindano hayo ambayo yataanza kutimua vumbi mapema mwaka huu.

 

Opa Clement Atoa Neno kwa Uongozi Simba SC

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa