Klabu ya Dodoma Jiji baada ya kupoteza mechi yao iliyopita, Leo hii watakuwa nyumbani kuwaalika Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro huku walima zabibu hao wakiwa na hali mbaya.

 

Dodoma Jiji Uso kwa Uso Dhidi ya Mtibwa Sugar.

Dodoma kwenye msimamo wapo nafasi ya mwisho ambayo ni ya 16, huku wakiwa wamecheza mechi 7, wameshinda mchezo mmoja pekee, wamepata sare mbili, wamepoteza michezo minne huku wakiwa wamejikusanyia pointi 5.

Mtibwa Sugar wao wapo nafasi ya 5 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo nane, ushindi mara tatu, sare mara tatu wamepoteza michezo miwili na wana alama 12 mpaka sasa huku wakitoka kushinda mechi yao iliyopita.

Ligi kuu ya NBC msimu huu imekuwa na ushindani wa hali ya juu huku kila timu ikijitahidi kadri ya uwezo wake iweze kupata matokeo mazuri na hatimaye waweze kusalia kwenye Ligi huku Azam ikiwapatia fedha vilabu vyote ambavyo vinashiriki Ligi ili iweze kuwasiaidia katika sekta mbalimbali ikiwemo usajili.

Dodoma Jiji Uso kwa Uso Dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo klabu hiyo ya Dodoma iliamua kuachana na kocha wao na sasa yupo kocha Melis Medo ambaye  huenda akabadilisha chochote katika timu yao. Na mchezo wa leo anauhitaji kwa hali na mali lakini swali liatakuja je ataweza kuchukua alama tatu mbele ya Walima Miwa?

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa