BAADA ya kuteuliwa kuwa Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe ameahidi kufanya kazi kwa ubunifu mkubwa ndani ya klabu hiyo.
Kamwe ambaye alikuwa mchambuzi wa soka alitangazwa jana akichukua nafasi ya aliyekuwa Ofisa Habari wa klabu hiyo ambaye mkataba wake ulimalizika, Hassan Bumbuli.

Akizungumza baada ya kuteuliwa Kamwe alisema kuwa “Namshukuru Mungu kupata nafasi hii ya kuitumikia klabu kubwa kama Young Africansa na nimefurahi sana.
“Ni changamoto mpya kwa upande wangu lakini ninawaahidi mashabiki na wanachama wote wa Yanga kufanya kazi kwa ubunifu na weledi mkubwa katika kuhakikisha mipango ya klabu inafanikiwa.”Afisa Habari wa Young Africans-Ali Kamwe
