VIJANA wapya wa Yanga kazini Ali Kamwe na Privadinyo kwenye idara ya Habari na Mawasiliano wametambulishwa rasmi jana Septemba 27.

Kamwe ni mchambuzi na mwandishi wa Habari za Michezo sawa na ilivyo kwa Privadinho ambao wote ni familia ya waandishi wa Habari.

 

Vijana Wapya Yanga Kazi Kazi

Pia Haji Mfikirwa yeye atakuwa kwenye kitengo cha fedha wakiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Yanga.

 

Vijana Wapya Yanga Kazi Kazi
Andrew Mtine ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Yanga naye ametambulishwa pia hivyo anaanza kazi na safu mpya kwenye idara ya habari.

Ni Haji Manara yeye ni Ofisa Habari wa Wananchi lakini amekuwa kando kutokana na kufungiwa miaka miwili huku Hassan Bumbuli akiwa hajaongezewa mkataba baada ya kumaliza kandarasi yake Agosti.

 

Vijana Wapya Yanga Kazi Kazi

Wote kwa pamoja wameanza kazi ya kuwahamasisha wapenzi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwenda kujitokeza kwa wingi viwanjani kuusaka ushindi kwenye mechi zote muhimu ikiwemo ile Al Hilal Oktoba 8.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa