Ali Kamwe: Kila kitu safi usemaji Yanga

KUNA kila dalilia kuwa mwandishi wa Habari za michezo na mchambuzi maarufu wa mchezo huo kwa sasa kutoka Azam TV, Ali Kamwe anakwenda kuwa msemaji mpya wa Yanga akichukua nafasi ya Haji Sunday Manara.

 

kamwe

Ali Kamwe, anakwenda kurithi nafasi ya usemaji wa klabu hiyo baada ya Manara kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili kufuatia kutofautiana na Rais wa TFF  Walace Karia miezi mitatu iliyopita.

Manara alionekana kwenye vipande vya video vikimuonyesha akizozana na Karia kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Azam kule Arusha, Yanga wakiwa wanacheza na Coastal Union kutoka Tanga na Yanga kufanikiwa kuwa bingwa kwa penalty 4-1.

Yanga baada ya kukaa muda mrefu bila kuwa na msemaji na pasipo na matarajio ya jambo la Manara kumalizika, wakafikia maamuzi ya kutoa nafasi ya watu wenye sifa kugombea nafasi ya usemaji kwenye klabu hiyo.

 

Ali Kamwe: Kila kitu safi usemaji Yanga

Juma Ayo kutoka Valor Tv, Twalib Muwa wa EFM, Jimmy Kindoki, ambaye ni shabiki nguli wa timu hiyo ya Yanga, Priva Abiud Shayo maarufu kama Privaldinho na Ali Kamwe walitajwa kuomba nafasi hiyo ya usemaji na Interview ikafanyika.

Sasa baada ya muda wa takribani wiki mbili kupita, umefika wakati wa Yanga kutangaza mshindi na tetesi nyingi zinadai kuwa Ali Kamwe amewashinda wenzake kwa sifa na anakwenda kutangazwa muda wowote kuwa mrithi wa Manara.

 

Ali Kamwe: Kila kitu safi usemaji Yanga

Mmoja ya watu ambao waliwahi kuwania nafasi hiyo ya usemaji na Ali, Twalib Muwa amekuwa akichapisha machapisho mengi ya kuhusu Ali kushinda nafasi hiyo kubwa kwa sasa kwenye soka la Tanzania.

Mbali na chapisho hilo, moja ya chanzo kutoka ndani ya Yanga ambacho akikutaka jina lake kuwekwa hadharani lilisema kuwa ni swali la muda tu kwa Ali Kamwe kutangazwa kuwa msemaji wa Yanga.

 

Ali Kamwe: Kila kitu safi usemaji Yanga

Pengine huo pia, ukawa mwisho wa Haji Manara kwenye nafasi hiyo ya usemaji na uzuri ni kwamba kwenye moja ya mahojiano aliyofanya hivi karibuni, Manara alifichua kuwa anafikiria kuachana na usemaji.

Acha ujumbe