Haji Manara ; Sihitaji Huruma ya Mtu Kwenye Jambo Hili

MSEMAJI wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa hahitaji kupata huruma kutoka kwenye mamlaka kutokana na kuweza kupewa adhabu ya kufungiwa miaka miwili pamoja na adhabu ya faini ya milioni 20 bali anahitaji haki.

Haji Manara
Haji Manara

Julai 21,Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) iliweka wazi kuwa imemfungia Manara miaka miwili pamoja na adhabu ya milioni 20 kutokana na kukutwa na hatia ya kumdhalilisha na kumdhihaki Rais wa TFF, Wallace Karia.

Haji Manara amebainisha kuwa anatambua na kuheshimu mamlaka ambazo zipo lakini ambacho anahitaji ni haki na hahitaji kuonewa huruma kwa kile ambacho kinatajwa kwamba yeye amekifanya.

“Nimepwa hukumu ambayo ninadhani ni kubwa kuliko kuwahi kutokea kwa hivi kariuni kwenye ulimwengu wa mpira hasa adhabu ya faini ina maana kwamba nimefanya kosa kubwa kweli na la kutisha.

Haji Manara
Haji Manara

“Lakini yote haya hata mchango mdogo ambao nimeufanya kwenye mpira nadhani upo ikiwa ni pamoja na kuwa kwenye Kamati ya Hamasa ya Timu ya Taifa lakini nafanya yote haya sio kuomba huruma hapana ninataka haki iweze kutendeka.

“Ninajua kwamba sijafanya jambo baya na kama ikitokea basi acha iundwe kamati huru katika hili na ikitokea nikakutwa nimefanya makosa basi nipo tayari kufungwa jela miaka 10,” amesema.

 

Kwa video za Uchambuzi wa michezo na ofa za Meridianbet Gusa Video Hapo Chini.


Acha ujumbe