MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amefunguka kuwa bao ambalo alifunga kiungo wa Yanga Feisal Salumu kwenye mchezo wa nusu fainali ya FA kwa shuti kali bado linamtesa hadi leo.

fei toto
fei toto

Ahmed alisema kwenye tukio ambalo lilitokea msimu uliopita kwenye ligi na likiwa linawahusu Simba basi ni kufungwa na Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba kwa kuwa kipigo hicho kiliwanyima kila kitu msimu uliopita.

Akizungumza juu ya goli hilo la Fei Toto Ahmed alisema: “Kusema ukweli kila nikivuta kumbukumbu ya kile kilichotokea msimu uliopita basi kumbukumbu mbaya ni juu ya goli la Feisal Salum Fei Toto ambalo lilifanya Simba sasa tupoteze kila kitu msimu uliopita.

“Ule ulikuwa ni mchezo wa nusu fainali ya FA, mchezo ambao kwetu ulikuwa umebeba vitu viwili vikubwa. Moja kumfunga mtani na pili ni kuingia fainali na kwenda kutetea kombe letu la FA.

fei toto
fei toto

“Kwa bahati mbaya haikuwezekana na ni mchezo  ambao naukumbuka hadi leo hasa lile goli la Feisal.”

Kwa Video nyingi za uchambuzi na matukio ya kimichezo unaweza kugusa Video hii hapa Chini.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa