Kiungo wa klabu ya Barcelona Franck Kessie imeelezwa hana mpango wa kuondoka klabuni kama taarifa zilivyoeleza hapo mwanzo.

Kuna taarifa zilisambaa kua kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast hana furaha ndani ya klabu hiyo na ana mpango wa kuondoka klabuni hapo majira ya baridi mwezi Januari.kessieWakala wa kiungo Franck Kessie amezungumza na kusema hizo ni taarifa za uongo, Na ukweli ni kua mchezaji huyo hana mpango wa kuondoka klabuni hapo na ana furaha pia.

“Ni taarifa za Uongo, Uongo kabisa. Franck yuko na furaha ndani ya Barcelena na hana mpango wa kuondoka klabuni hapo” Wakala wa mchezaji huyo alisisitiza kwa namna hiyo juu ya madai hayo.kessieKiungo Franck Kessie amekua akipata wakati mgumu kupata nafasi chini ya mwalimu Xavi, Na amekua akicheza mara chache sana jambo ambalo limefanya kukaibuka kwa tetesi za namna hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa