Klabu ya Azam FC inatarajia kuikaribisha Ihefu hapo kesho kwenye mchezo wao wa Ligi kuu ya NBC baada ya kupata ushindi mechi iliyopita dhidi ya Simba katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa Chamazi Complex majira ya saa 1:00 ambapo Agrey Moris ambaye pia nae amepewa jukumu la kuismamia timu hiyo amesema kuwa wachezaji waote ni wazima na wamejipanga kuwakabili Ihefu.
Hakuishia hapo aliongeza kwa kusema kuwa hawezi akazungumzia mechi ambayo imepita bali wanatazama yajayo na kwasasa wanaangalia zaidi kuwajenga wachezaji kiakili ili waweze kupata ushindi.
Huku mchezaji wa Azam pia Sospeter Bajana amesema pia wamejipanga kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo.
Azam mpaka sasa kwenye msimamo wa ligi kuu wapo nafasi ya 5 baada ya kucheza mechi 8, wameshinda michezo minne, sare mbili na wamepoteza michezo miwili huku wakijikusanyia pointi 14.
Wakati kwa upande wa Ihefu wao bado mambo ni magumu huku wakiwa na pointi 5 pekee baada ya kucheza michezo 8 ushindi mara moja na kupoteza mara tano wakiambulia sare mbili tuu.