Hatimaye ile jezi ya staa bora wa Kimataifa wa Ureno na Manchester United Cristiano Ronaldo, imekabidhiwa kwa Uongozi wa timu ya Azam FC yenye maskani yake nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam- Chamazi.
Jezi hiyo ya Ronaldo yenye rangi nyekundi na saini ya mshambuliaji huyo, ilikabidhiwa mapema hii leo na Mtaalamu wa tiba za wachezaji wa AZAM FC João Pedro Rodrigues, ambapo jezi hiyo ilipokelewa na mmiliki wa timu hiyo Yusuf Bakhresa.
View this post on Instagram
Taarifa kutoka klabuni hapo ilitumwa kwenye ukurasa wa Instagram iliandika kuwa “Jezi hiyo maalum ya Manchester United, imesainiwa na staa huyo kwenye eneo la juu la namba saba mgongoni”
Azam FC ambao wametoka kuifunga Simba SC kwenye mchezo wa raundi wa 8 ya Ligi Kuu ya NBC siku ya Alhamis, wapo kwenye furaha hiyo ambapo kabla ya mchezo huo mmiliki wa timu Yusuf alizungumza na wachezaji na kuwapa hamasa kwenye mchezo huo.
Mchezo unaofuata wa Azam atakuwa mwenyeji dhidi ya Ihefu ya Jijini Mbeya, mchezo utakaopigwa kesho kwenye dimba la AZAM Complex.