Klabu ya Mbeya City baada ya kutoka kutoa sare mchezo uliopita, kesho anamkaribisha Tanzania Prisons katika mchezo wao wa 18 wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara majira ya saa 10:00.

Mbeya City amecheza mechi 7 mfululizo bila kupata pointi 3, huku kati ya hizo mechi amepoteza mbili. Mechi ya mwisho kushinda ilikuwa ni tarehe 4 Novemba aliyocheza dhidi ya Namungo.
Tanzania Prisons yupo nafasi ya 11 baada ya michezo 17 aliyocheza, akishinda mechi zake nne, sare sita na kupoteza mara saba hadi sasa, huku akijikusanyia pointi zake 18 tuu.

Mbeya City yupo nafasi ya 10, wakiwa wametofautiana pointi tatu pekee huku Wanakoma Kumwanya wakikusanya pointi zao 21 baada ya michezao 17 waliyocheza, ushindi wamepata mara nne, sare 9 na kupoteza mara nne.
Mechi 5 za mwisho kukutana kati ya hizi timu mbili wameenda sare mara nne huku mechi moja Mbeya akiibuka na ushindi mwembamba. Je kesho nani kuondoka na pointi 3 au ni kugawana pointi tena?

