Mchezo mwingine wa Ligi kuu ya NBC unaotarajiwa kupigwa leo ni ule unaowakutanisha kati ya Mbeya City dhidi ya Singida Big Stars majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Sokoine Mbeya.

Mbeya City amecheza michezo yake 16, kashinda mechi zake nne, kasare mechi nane na kapoteza nne vilevile akijikusanyia alama 20 kibindoni hadi sasa, anashikilia nafasi ya 9 kwenye msimamo.
Wakati Singida wao wapo nafasi ya nne ambayo ni nafasi nzuri ambayo kama akiendelea kuwa na ubora ataweza kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho msimu ujao. Ndani ya michezo 16 ameshinda 9, kaenda sare tatu na kapoteza mara nne pointi 30.
Mbeya City wao wametoka kupoteza mchezo wao uliopita, huku Singida wao wametoka kushinda mechi yao iliyopita huku leo kila timu ikizihitaji pointi hizo ili aweze kukaa kwenye nafasi nzuri.

Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili Singida alishinda. Je leo hii Mbeya atakubali kichapo kingine kutoka kwa walima alizeti wa Singida?

