Benchi la ufundi la Mbeya City limeweka wazi kuwa hawana mpango wa kumrudisha kwenye timu yao, Kibu Denis.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya klabu ya Simba kabla ya kujiunga nao alikuwa akikitumikia kikosi cha Mbeya City kwa mafanikio makubwa.

Mbeya City yamkana Kibu Denis

Akizungumzia hilo, Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amesema “Kwanza benchi la ufundi halijatoa mapendekezo yeyote juu ya usajili.

“Labda hilo lipo kwa Uongozi lakini kwa sasa kocha amesafiri kwenda kuisalimia familia yake hivyo tunamsubiri akifika yeye ndio atatoa mapendekezo yake.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa