Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi imewafungia wachezaji watatu wa Pan African kucheza kwenye mechi tatu na kuwatoza faini ya laki tano (500,000) kila mmoja.

Wachezaji hao ni Diey Makonga, Patrick Muhagama na Abdallah Rashid ambapo adhabu hiyo ilitolewa jana jumatano na bodi ya ligi.

Watatu (03) Pan waipa TFF Mil 1.5

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi ilieleza kuwa sababu za kufungiwa kwa wachezaji hao ni kuwashambulia waamuzi wa mchezo kati ya Ken Gold dhidi ya timu hiyo kwa matusi na maneno yasiyo ya kiungwana.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya ulimalizika kwa Pan kupoteza kwa mabao 5-2.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa