Uongozi wa Pan African leo umetangaza kuwasimamisha nyota wake sita kutokana na utovu wa nidhamu.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau ilieleza kuwa “Tunapenda kuwataarifu wanachama, wapenzi na mashabiki wetu na wapenda soka kuwa tumewasimamisha wachezaji wetu sita kutokana na utovu wa nidhamu.

Nyota sita wasimamishwa Pan African
“Wachezaji hao ni Bakari Jomba, Patrick Muhagama, Thadei Ally, Diey Makonga, Mathias Jezalian na Maulid Dege.

“Tumewasimamisha kwa muda mpaka pale uongozi utakapojiridhisha juu ya mabadiliko yao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa