Rais wa zamani wa shirikisho la soka barani Ulaya na gwihi wa zamani wa soka la Ufaransa Michael Platini amefurahia timu yake kutinga hatua ya fainali kwa mara ya pili mfululizo.

Timu ya taifa ya Ufaransa jana imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wa nusu fainali kwa mabao mawili kwa bila.platiniKupitia mwanasheria wake inaelezwa Michael Platini amejiskia ufahari na furaha kubwa baada ya Ufaransa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa mara ya pili mfululizo na kufanikiwa kuweka rekodi kwenye michuano hiyo.

Gwiji huyo ambaye aliwahi kubeba taji la ulaya na timu ya taifa ya Ufaransa akiwa na kizazi cha dhahabu mwaka 1984, Ambapo gwiji huyo anasema hata kizazi chao cha dhahabu hakikuweza kufikia ubora ambao wameonesha sasa kwenye michuano hiyo.

Michael Platini alikua kwenye kamati ya maandalizi mwaka 1998 ambapo michuano ilifanyika Ufaransa na kufanikiwa kua bingwa wa michuano hiyo, Lakini alishindwa kushiriki mwaka 2018 nchini Urusi Ufaransa wakiwa mabingwa kwakua alikua akitumikia kifungo baada ya kukiuka taratibu wakati akiwa rais wa Uefa.platiniTimu ya taifa ya Ufaransa kwasasa inafukuzia rekodi ya kua timu ya kwanza kubeba taji hilo mara mbili mfululizo baada ya Brazil kufanya hivo mwaka 1958 na 1962, Hivo Ufaransa wakibeba taji hilo siku ya jumapili wanafikia rekodi hiyo kwakua watakua wamebeba mwaka 2018 na 2022.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa