Platini:Benzema Anapaswa Kuthibitisha Ushindi Wake Kombe la Dunia.

Rais wa zamani wa shirikisho la soka ulaya na mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Michael Platini amemtaka staa wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema kuthibisha ushindi wake wa Ballon Dor kwenye kombe la dunia.platiniKarim Benzema ambae amekabidhiwa tuzo ya Ballon Dor juzi usiku baada ya kua na msimu bora kabisa baada ya kumaliza kama mfungaji bora wa La liga na ligi ya mabingwa ulaya na kuisaidia klabu yake mataji matatu ikiwemo ligi ya mabingwa ulaya.

Platini anaamini Benzema anahitajika kuonesha ubora mkubwa katika michuano ya kombe la dunia ili kuhalalisha tuzo yake aliyokabidhiwa juzi usiku gwiji huyo wa zamani wa Ufaransa anaamini staa huyo akionesha ubora mkubwa kwenye michuano hiyo hakuna atakayenyoosha kidole kuhoji ubora wa staa huyo.platiniBenzema anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu ya taifa ya Ufaransa katika michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kupigwa nchini Qatar mapema mwezi Novemba.

Benzema anaungana na magwiji kutoka Ufaransa kama Michael Platini na Zinedine Zidane ambao wameshawahi kutwaa tuzo ya Ballon Dor.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.