Staa wa klabu ya Psv Eindhoven na timu ya taifa ya Uholanzi Coady Gapko amefunguka namna ambavyo alikaribia kujiunga na mimba ya soka nchini Uingereza klabu ya Manchester United.
Staa huyo wa klabu ya Psv alikua ni miongoni mwa wachezaji waliokua wanafatiliwa kwa karibu na klabu ya Manchester United kabla ya dili hili kuvunjika mwishoni na mchezaji huyo kusalia katika klabu ya Psv.
Coady Gapko amefanya mazungumzo na kueleza alikaribia kuondoka klabuni hapo na timu ambayo alikua anaelekea kwa kiwango kikubwa sana ni Man United kwani amedai kufanya mazungumzo mara kadhaa na kocha wa klabu hiyo Eric Ten Haag.
“Nilizungumza na Ten haag mara kadhaa, Lakini mwisho dili halikufanikiwa jambo ambalo lilikua la aibu” “Manchester United ni klabu kubwa duniani” Coady Gapko amekua miongoni mwa mchezaji aliehusika kwenye magoli mengi msimu huu akiwa sambamba na mshambuliaji wa Manchester City.
Dili la Gapko inaelezwa lilifeli kutokana na kusajiliwa kwa winga wa klabu ya Ajax raia wa Brazil Antony Santos baada ya kumpata winga huyo ulisababisha dili la mchezaji huyo kufa lakini bado Man United imemuweka kwenye mipango yake staa huyo wa kiholanzi

