Neymar Jr Azipa Nafasi Ufaransa na Argentina Kombe la Dunia.

Staa wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya PSG inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Neymar Jr amezipa nafasi timu za Ufaransa na Argentina kuelekea kombe la dunia nchini Qatar mapema mwezi ujao.

Baada ya Neymar Jr kuzungumza timu anazoziona zikifanya vizuri kombe la dunia imeibua hisia tofauti kwa wadau wa soka wengine wakikubaliana na maoni hayo ambayo ameyatoa sta huyo huyo wa klabu ya PSG.neymar jrTimu ya taifa ya Brazil na Argentina ni timu nzuri na zenye wachezaji mahiri kwenye vikosi vyao hivo haijashangaza watu kuona amezipa nafasi timu hizo staa huyo wa kimataifa wa Brazil.

Lakini kwenye timu ya taifa ya Ufaransa kuna laana imekua ikiwatafuna mabingwa wa kombe la dunia kutokufanya vizuri katika michuano inayofata kwani hata Ufaransa wenyewe kabla ya kubeba kombe la dunia mwaka 2018 walibeba kombe hilo mwaka 1998 michuano iliyofata mwaka 2002 walitokea makundi.neymar jrHali hiyo inawafanya watu kuamini kumekua na laana ambayo imekua ikiwatafuna mabingwa wa kombe na kiwango cha siku za karibuni cha timu ya taifa ya Ufaransa kinatia wasiwasi kuelekea Qatar na wadau wa soka wakiona laana inaweza kuendelea kwa mabingwa hao watetezi.

Pamoja na Neymar Jr kuzipa nafasi timu hizo lakini ni ukweli usiofichika kua timu ya taifa ya Brazil ni miongoni mwa timu bora na zinazotazamiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia mapema mwezi ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.