Staa wa klabu ya PSG na timu taifa ya Brazil Neymar Jr amempongeza staa wa klabu ya Real Madrid aliefanikiwa kubeba tuzo ya Ballon Dor usiku wa kuamkia jumatatu nchini Ufaransa.
Neymar Jr amesema anaona kabisa Karim Benzema amestahili kupewa tuzo hiyo akiandika katika mtandao wake wa Twitter ameonesha kukubali staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa kupewa tuzo hiyo.
Karim Benzema ambae alitangazwa kua mchezaji bora wa dunia kupitia tuzo zinazodhaminiwa na jarida la Ufaransa linalojulikana kama France Football za Ballon Dor baada ya kua na msimu bora sana kwenye msimu wa 2021/22 baada ya kua mfungaji bora wa ligi ya mabingwa ulaya, La liga huku akiisaidia klabu yake ya Real Madrid kubeba mataji kadhaa.
Watu wengi wameoneshwa kufurahishwa na kitendo cha staa huyo wa Brazil kumpongeza Benzema kubeba tuzo hiyo huku wakiwa wanatoka timu tofauti hii imefanya watu kumuona Neymar Jr ni mtu muungwana.
Neymar mbali na kumpongeza Benzema lakini alionesha kusikitishwa na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Real Madrid Vinicius Jr ambaye alitangazwa kama mchezaji namba nane kitu ambacho staa huyo wa Brazil hakuona ni sahihi.
Neymar Jr aliandika pia kwenye mtandao wa Twitter kua Vinicius Jr alistahili kua kwenye tatu bora ya tuzo hizo na kuwekwa namba nane ni jambo ambalo Neymar hajakubaliana nalo.

