Pogba Arejea Mazoezini Ndani ya Juventus.

Nyota wa klabu ya Juventus Paul Pogba amerejea mazoezini ndani ya klabu hiyo baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyokua yakimsumbua.paulNyota huyo wa zamani wa Manchester United hakuwahi kushiriki mechi yeyote ya kimashindano na klabu yake hiyo mpya baada ya kupata majeraha ya goti lake la kulia ambayo yamekua yakimsumbua kwa muda mrefu.

Kurejea kwa Pogba katika kiwanja cha mazoezi ni habari nzuri kwa klabu ya Juventus chini ya mwalimu Massimiliano Allegri kwakua timu hiyo imekua ikifanya vibaya hivi karibuni na urejeo wa kiungo huyo unaweza kua sehemu ya kuleta uhai kwa timu hiyo.pogbaPia kupona kwa Pogba ni furaha pia kwa timu ya taifa ya Ufaransa ambapo zimebaki wiki tano kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar na mabingwa watetezi hao walikua wakimuhitaji kiungo huyo kwa kiwango ili kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo.

Pia kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps ameonesha kufurahishwa na urejeo wa kiungo baada ya majeruhi ya muda mrefu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.