Man United Kutupa Karata yao Dhidi ya Spurs Leo.

Klabu ya Man United leo itakua dimbani kuwaalika klabu ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.man unitedManchester United ambao wamekua hawapo kwenye kiwango bora sana katika mechi za hivi karibuni wanaenda kucheza na Tottenham ambao wapo kwenye kiwango kizuri huku wakishika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Mashetani wekundu hao leo watajitupa uwanjani huku wakiwa wamevuna alama nne katika michezo yao mitatu ya mwisho hivo ikionesha mwenendo sio mzuri ndani ya timu lakini kuelekea mchezo huo rekodi zinawabeba klabu hiyo.

Tottenham wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya kwani msimu uliomalizika walipoteza michezo yote miwili dhidi ya klabu ya Man United katika ligi michezo ya ligi kuu ya Uingereza.man unitedMchezo huu utakwenda kurudisha matumaini kwa Man United kama watafanikiwa kushinda mchezo na kujiamini kwani mchezo unaofuata wa ligi kuu Uingereza watamenyana na klabu ya Chelsea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.