Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United na klabu ya Bayern Munich Bastian Schweinsteiger amesema mshambuliaji wa klabu hiyo Anthony Martial atakua bora sana kaama ataamini katika ubora wake.

Kiungo huyo mshindi wa kombe la dunia na timu ya taifa ya Ujerumani nchini Brazil mwaka 2014 alikuepo wakati Martial anawasili Manchester United kwa mara ya kwanza mwaka 2015, Hivo anaamini katika ubor wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.schweinsteigerBastian Schweinsteiger wakati akifanya mahojiano na Televisheni ya Man United amesema mshambuliaji Martial ana ubora mkubwa kwani anakumbuka wakati amekuja klabuni hapo na kufunga bao zuri dhidi ya Liverpool, Hivo akaeleza kuna muda ubahitajika kumpa kujiamini na pia kumfanya apambane zaidi kitu kinachoweza kumfanya kua bora zaidi.

Gwiji Schweinsteiger ameeleza pia kocha na wachezaji wenzake wanatakiwa kumsaidia mchwzaji huyo kua bora zaidi, Kwani wakati yeye anacheza nae alijitahidi kumpa mipira wakati sahihi uwanjani ili aweze kuonesha ubora wake.schweinsteigerAnthony Martial alionesha ubora mkubwa wakati wa kujiandaa na msimu mpya huku akioneka kumvutia kocha wa klabu hiyo Eric Ten Hag, Lakini majeraha yamekua changamoto kubwa mchezaji huyo kuendeleza makali yake aliyoayaonesha katika mechi za kujiandaa na msimu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa