Shweinsteiger: Ujerumani ina Beki mmoja Mwenye Ubora wa Dunia

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich Bastian Shweinsteiger amesema timu ya taifa ya Ujermani ina beki mmoja tu ambae ana ubora wa kiwango cha dunia.

Shweinsteiger ameyazungumza hayo baada ya timu hiyo kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia hapo jana huku akimtaja Antoni Rudiger kama beki mwenye ubora wa juu kwenye kikosi hicho cha mwalimu Hans Dieter Flick.schweinsteigerKwenye michezo yote mitatu ya hatua ya makundi ambayo timu ya taifa ya ujerumani imecheza imeruhusu magoli hivo inaonesha kwa namna gani timu hiyo imekua na safu mbovu ya ulinzi na kiungo huyo anaiona kama ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kutolewa kwenye michuano hiyo mapema.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kimetolewa kwenye michuano ya kombe la dunia kwenye hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kutolewa kwenye hatua hii mwaka 2018 na mwaka huu imejirudia tena. Hii inaonesha ubora wa timu hiyo umeshuka kwa kiwango kikubwa.schweinsteigerBastian Schweinsteiger ni wazi akiiangalia safu ya ulinzi ya timu hiyo anaona inakosa ubora kwa kiwango kikubwa kutokana na namna timu hiyo ilikua ina ukuta wenye ubora miaka kadhaa nyumani wakati yeye mwenyewe alikua anaitumikia timu hiyo.

 

Acha ujumbe