Beki wa klabu ya Rb Leipzig inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani pamoja na timu ya taifa ya Croatia Josko Gvardiol amefunguka kua klabu ya Real Madrid ni klabu kubwa duniani na huenda akacheza klabu hiyo siku moja.
Beki huyo ambaye anaonekana yupo kwenye ubora mkubwa kwasasa amefunguka kuhusiana na klabu ya Real Madrid na hii ni baada ya kufanya mahojiano na wanahabari kuhusiana na klabu hiyo “Real Madrid ni klabu kubwa zaidi duniani. Nani anajua naweza kwenda kucheza pale siku moja” Alisema Josko
Beki huyo amekua akihusishwa na vilabu vikubwa barani ulaya kama Real Madrid pamoja na klabu ya Chelsea kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha . Beki huyo ambaye kwasa aanashiriki michuano ya kombe la dunia na akisimama kama nguvu muhimu sana kwenye safu ya ulinzi ya Croatia.
Pia Josko Gvardiol amefunga kua amekua akiongea na nyota mwenzake wa timu ya taifa ya Croatia Luca Modric na kueleza “Modric hana haja ya kunieleza kitu chochote kuhusu Real Madrid kwasababu najua kila kitu kuhusu Madrid kwakua ni klabu kubwa, Na pia najjua umuhimu wa kuhusishwa na klabu kama Real Madrid” Alisema Gvardiol.
Beki huyo ameeleza anafurahishwa kuhusishwa na klabu kubwa lakini kwasasa anafurahia maisha ndani ya klabu Red Bull Leipzig ya nchini Ujerumani.

