Timu ya taifa ya Ghana na Uruguay ambazo zimecheza pamoja katika mchezo wa mwisho wa kundi H jioni ya leo wamejikuta wote wakiwa nje ya michuano ya kombe la dunia.
Licha ya Uruguay kuifunga timu ya taifa ya Ghana kwa jumla ya mabao mawili kwa bila na kuwafanya alama 4 lakini haikua sababu ya kuwafikisha kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo baada ya Korea Kusini kushinda dhidi ya Ureno.Timu ya taifa ya Ureno ambayo ilishafuzu hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Uruguay kwa mabao mawili kwa bila katika mchezo wa pili wa kundi hilo, Leo wamekubali kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Korea ya Kusini na kuifanya timu hiyo kufuzu baada ya kufikisha alama nne.
Korea Kusini wamefikisha alama nne baada ya kuifunga Ureno sawa na timu ya Uruguay lakini Uruguay wanatoka kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kwani Korea Kusini wamefunga magoli mengi zaidi.Ghana wao wanashindwa kulipiza kisasi dhidi ya timu ya taifa ya Uruguay baada ya kukubali kupokea kipigo cha mabao mawili kwa bila katika mchezo huo dhidi ya Uruguay huku historia ikijirudia baada ya Andre Ayew kukosa Penati mapema kabisa kwenye nchezo huo.
Ghana wanaondoka kwenye michuano hiyo wakiwa na alama tatu pekee walizozipata katika mchezo wa pili dhidi ya Korea Kusini. Timu hiyo inakua timu ya pili kutoka Afrika kuenguliwa kwenye michuano hiyo baada ya Tunisia.