Timu ya taifa ya Korea Kusini imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Ureno kwa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa mwisho kundi H.
Timu hiyo baada ya kushinda dhidi ya Ureno imefanikiwa kufikisha alama 4 ikiwa sawa na timu ya taifa ya Uruguay ambao pia nao wamefikisha alama nne baada ya kuifunga Ghana kwa mabao mawili kwa bila.
Timu ya taifa ya Korea Kusini inaungana na timu ya taifa ya Ureno kufuzu hatua ya 16 kwenye kundi H baada ya kuongoza kwenye magoli ya kufunga kwani walilingana magoli a kufunga na kufungwa na Uruguay, Lakini timu hiyo kutoka bara Asia iliongoza kwa magoli mengi ya kufunga ikiwa imefunga mabao manne huku Uruguay ikiwa imefunga mabao mawili pekee.
Ikumbukwe timu ya taifa ya Ureno ilishafuzu baada ya kushinda michezo yake miwili ya awali hivo hata kupoteza kwao leo hakujaharibu kitu kwakua walishafuzu na wamefanikiwa kubaki kileleni kwenye msimamo wa kundi lao.
Timu ya taifa ya Korea Kusini baada ya kufanikiiwa kufuzu hatua ya mtoano ni wazi kuna asilimia kubwa ya kukutana na timu ya taifa ya Brazil kwenye hatua hiyo kwani Brazil mpaka sasa anaongoza kundi G ambapo atakutana na mshindi wa pili kundi H.

