Kutokana na kuporomoka kwa maambukizi mapya ya wagonjwa wa COVID 19 nchini Korea Kusini, mechi za mpira wa miguu zimeruhusiwa kuanza leo. ambapo vilabu vimeruhusuwa kucheza mezi zao bila mashabiki na mechi hizo zitakua za kirafiki na zitahusisha watu walio salama kwa maana ya kutokua na dalili za janga la Korona (Covid19).

Vilabu vya Korea Kusini vitaweza kucheza mechi hizo, kama ilivyotangazwa na Chama cha Soka cha Korea Kusini, ambapo bado hakijaweka wazi tarehe rasmi ya kuanza msimu mpya.Mechi za kirafiki zitafanyika sio tu kwa kutokuwepo kwa mashabiki lakini pia media chache zitaruhusiwa kurusha matangazo.
Ligi Kuu ilipangwa kuanza tarehe 29 Februari, lakini iliahirishwa kwa sababu ya janga la coronavirus ambalo katika kipindi hicho lilikuwa katika kilele cha maambukizi huko Korea Kusini. Soka sio mchezo tu utakaoanza lakini pia kuanzia Mei 5 mechi za ‘baseball’ zitaendelea tena, ikumbukwe ni mojawapo ya mchezo maarufu sana katika nchi za Asia.
Kulingana na data za hivi karibuni kutoka Vituo vya Korea vya Kudhibiti na Kuzuia Corona, Korea jana kulikuwa na kesi tisa tu za maambukizi nchini, tano zilitoka nje ya nchi na zaidi.


lombo
saf mambo n motoooo