Timu ya taifa ya Cameroon itashuka dimbani usiku huu kutafuta nafasi kufuzu hatua ya 16 bora dhidi ya timu ya taifa ya Brazil ambao tayari wameshafuzu hatua hiyo baada ya mechi zake mbili za awali.

Timu ya taifa ya Cameroon chini ya mwalimu Rigobert Song wao mpaka wakati huu hawafjafanikiwa kushinda mchezo hata mmoja kati ya miwili waliyocheza huku wakiambulia sare na kufungwa mchezo mmoja.cameroonSimba wasiofugika leo watakua wanahitaji alama tatu muhimu huku wakiwaombea timu ya taifa ya Uswisi matokeo mabaya kwani mpaka sasa Uswis wana alama tatu ambazo walizipata dhidi yao.

Timu ya taifa ya Brazil leo wanaweza kuamua hatma ya Cameroon kama wakipoteza dhidi ya Simba wasiofugika huku timu hiyo ikiwa na kazi ya kuomba matokeo mabaya kwa timu ya taifa ya Uswisi ikiwezekana wapoteze kwa goli moja huku wao wapate ushindi wa zaidi ya goli moja.cameroonMchezo wa Serbia na Uswisi pia utakua na nafasi kubwa ya kuamua kama Cameroon atakwenda hatua inayofuata kwani hata ikitokea Cameroon anashinda halafu Uswisi nae anashinda haitakua na faida kwa upande wao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa