Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amefunguka kuwa kila timu kwenye makundi ya hatua ya michuano ya Klabu bingwa Afrika inapaswa kuheshimiwa.

Timu hiyo imepangwa kundi C kwenye michuano hiyo ikiwa na timu za Horoya AC, Raja Casablanca na Vipers.

Mgunda atoa neno makundi ya CAF

Akizungumzia kundi lao, Mgunda alisema “Tulifuzu hivyo tulichokuwa tunakisubiri ni kupangiwa timu gani ambazo tutaenda kukutana nazo.

“Tunapaswa kuziheshimu timu zote katika kundi letu hivyo tunawaomba mashabiki wetu watuunge mkono katika kuhakikisha tunaingia hatua ya robo fainali.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa