Wakitarajia kuivaa Eagle FC kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kesho nyota, Kibu Denis amerejeshwa ndani ya kikosi cha Simba.

Mchezo huo wa ASFC unatarajiwa kupigwa kesho jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo Simba watakuwa wenyeji.

Kibu Denis arejea kikosini Simba

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema “Kikosi kimeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Eagle FC.

“Ni mechi rahisi lakini pia ni mechi ngumu kwani hatuwafahamu wapinzani wetu kama wao wanavyotufahamu sisi lakini itakuwa aibu Simba kutolewa na timu ndogo kama Eagle.

Kibu Denis arejea kikosini Simba

“Wachezaji wote wapo fiti na baadhi yao wamerejea kikosini ambao ni Nelson Okwa ambaye alikuwa majeruhi na Kibu Denis ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia.

“Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa Mkapa kesho wafanye kuwa mtoko wa familia kuja kukiona kikosi chao na kufurahi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa