Cristiano Ronaldo hajawahi kuomba kuondoka kwenye kikosi cha Ureno kwenye Kombe la Dunia, lakini kocha Fernando Santos alikiri kwamba mshambuliaji huyo mkongwe hakufurahishwa na kutoanza kwenye mechi dhidi ya Uswizi.

 

Santos: "Ronaldo Hakuomba Kuondoka kwenye Kambi ya Ureno"

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliachwa kwa mchuano wa hatua ya 16 bora na Uswizi huku Ureno ikiibuka na ushindi wa 6-1 ambapo mchezo wa robo fainali watamenyana dhidi ya Morocco hapo kesho.

Ripoti zilidokeza kuwa kulikuwa na mzozo mkubwa kati ya Santos na Ronaldo huku Ronaldo akitishia kuondoka, lakini hilo lilikataliwa kabisa.

Santos alisema: “Tulifanya mazungumzo. Sifanyi hivyo na wachezaji wote lakini yeye ni nahodha wa kikosi. Unajua anawakilisha nini kwa soka la Ureno, kwa watu wa Ureno na kwa timu ya taifa.”

Kocha huyo anaongeza kwa kusema kuwa alimweleza baada ya chakula kuwa kwanini hatocheza na kulingana na mkakati wao anadhani itakuwa bora kama asingeanza kwani anadhani mchezo utakuwa mgumu na yeye itamuokoa.

Santos: "Ronaldo Hakuomba Kuondoka kwenye Kambi ya Ureno"

Lakini ni wazi Ronaldo hakuwa na furaha sana kwani amezoea kuanza kwenye kikosi cha kwanza na walikuwa na mazungumzo ya kawaida ambayo alielezea pointi zake na akakubali.

“Hakuwahi kuniambia anataka kuondoka kwenye timu ya taifa.”

Santos mara nyingi huvaa sura ya mtu aliyekasirika lakini alishangazwa hasa na maswali ya mara kwa mara yanayohusiana na nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid.

Santos: "Ronaldo Hakuomba Kuondoka kwenye Kambi ya Ureno"

Santos anasema kuwa ni wakati muafaka wa kuachana na mazungumzo haya na kuangalia kile alichokifanya kwenye mechi. Mchezaji mbadala wa Ronaldo dhidi ya Uswizi, Goncalo Ramos, alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ akiwa sehemu ya timu iliyoonyesha uwezo mkubwa wa kushambulia kuliko mechi zilizopita nchini Qatar.

Mchezaji mwingine Joao Felix alikuwa mwingine aliyeng’ara dhidi ya Uswizi, akicheza mchezo wake bora zaidi wa mashindano hayo.

Santos: "Ronaldo Hakuomba Kuondoka kwenye Kambi ya Ureno"

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa