Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kua vinara wa ufungaji mabao kwenye ligi kuu ya NBC mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika.

Wekundu hao wa msimbazi licha ya kukamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo lakini wameonesha umahiri wao kwenye kupachika mabao kwani mpaka sasa ndio timu iliyofunga mabao mengi zaidi kwenye ligi hiyo wakiwa na jumla ya mabao 31.simbaSimba wanaongoza kwa kufunga mabao wakiwa na mabao 31 lakini pia ukichukua uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa bado klabu hiyo inakua juu kwani inakua na magoli 24 ikifuatiwa na vinara Yanga wenye mabao 19 wanaoshika nafasi ya pili klabu ya Azam wakiwa na mabao 9.

Wekundu wa Msimbazi wameonesha safu yao ya ushambuliaji ni hatari na imeimarika tofauti na msimu uliomalizika ambapo walikua wanapata wati mgumu sana wa kuweka mpira wavuni kutokana na kua na safu ya ushambuliaji isiyo na makali.simbaInaelezwa klabu ya Simba licha ya kuongoza kwa mabao ya kufunga kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi kuu, Lakini viongozi wa klabu hiyo watanataka kuingia sokoni Januari kwenye didisha dogo na miongoni mwa sehemu zitakazoboreshwa ni pamoja na eneo la ushambuliaji.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa