Ligi kuu ya NBC kuendelea kesho ambapo ni Mzizima Derby inayowakutanisha kati ya Azam FC na Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi msimu uliopita.

Azam FC wapo nafasi ya tatu hadi sasa baada ya kucheza michezo yao 17, wamepata ushindi mara 11, sare nne na wamepoteza michezo miwili, alama zao 37 kibindoni hadi sasa.
Wakati Yanga wao wapo kileleni kwenye msimamo wakiwa wamejishindia mechi zao 14 kati ya 17, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja tuu, wakiwa na alama 44 tofauti pointi 6 na anayeshikilia nafasi ya pili.

Kaimu Afisa habari wa Azam Hasheem Ibwe amesema kuwa pointi zao tatu zitanzia kesho kwenye mechi yao itakayopigwa katika Uwanja wa Mkapa majira saa 2:15 usiku baada ya kupata sare mbili mfululizo.
Mechi ya kwanza kukutana msimu huu kwenye ligi timu zilitoshana nguvu kwa kutoa sare ya 2-2 huku Yanga akiwa ndiye anasawazisha mabao yote baada ya vijana wa Kally Ongala kutangulia kufunga.

