Klabu ya Azam Fc imelazimishwa sare na klabu ya Geita Gold katika mchezo wake wa pili mzunguko wa pili wa ligi kuu ya NBC mchezo uliopigwa katika dimba la Nyankumbu Mkoani Geita.

Klabu ya Azam ambayo ilikua ugenini leo iliuanza mchezo wake vizuri dhidi ya klabu ya Geita baada ya kuanza kupata bao la mapema kupitia mshambuliaji wake hatari Prince Dube, Na kuwapa uongozi klabu hiyo mpaka muda wa mapumziko.azamKipindi cha pili kiliendelea kwa vijana wa Kally Ongala kuonekana wanatafuta bao la pili ili kuimaliza mechi hiyo, Mpaka pale dakika ya 69 ya mchezo klabu ya Geita Gold walipopata mkwaju wa penati na kuwekwa kimiani na Offen Chikola na kufanya mchezo kua sare ya bao moja kwa moja.

Klabu ya Azam Fc sasa imedondosha alama nne katika mechi zake mbili za mzunguko wa pili ni baada ya kulazimishwa sare na klabu ya Kagera Sugar katika mchezo uliopita katika dimba lake la nyumbani la Azam Complex.

Matajiri hao wa jiji la Dar-es-salam sasa wanaendelea kutoa wigo kwa klabu ya Simba kujisimika katika nafasi ya pili ambayo walikua wakiishikilia kwa muda mrefu, Kama klabu ya Simba itashinda mchezo wake leo dhidi ya Kagera Sugar basi itafanikiwa kuwaacha klabu hiyo kwa alama tatu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa