Azam yaachana na Ajibu

Uongozi wa Azam FC umetangaza kuachana na nyota wake, Ibrahim Ajibu baada ya mkataba wake kumalizika.

Ajibu alijiunga na timu hiyo akitokea Simba baada ya kumaliza mkataba wake ambapo hakuweza kuonyesha kiwango kizuri ndani ya kikosi hicho.

Azam yaachana na Ajibu

Akiwa katika timu hiyo pia Ajibu hakuwa na kiwango kizuri baada ya kujiunga nao Desemba 30, 2021 kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Tetesi zinaeleza kuwa nyota huyo huenda akajiunga na klabu ya Polisi Tanzania au Singida Big Stars.

 

Acha ujumbe